FAHAMU FAIDA KUMI 11 ZA KIAFYA ZITOKANAZO NA TANGAWIZI



FAHAMU FAIDA KUMI 11 ZA KIAFYA ZITOKANAZO NA TANGAWIZI



1. Huondoa Harufu mbaya ya kinywa.
Tofauti na vyakula vingine kama kitunguu swaumu, tangawizi husaidia uwe na harufu nzuri pale unapopumua na kufanya maeneo yamdomo kuwa safi.

2.  Msukumo Wa Damu
Tangawizi husaidia msukumo wa damu mwilini kwasababu huupa mwili joto ambalo mara nyingi mwili huhitaji wakati wa usukumwaji wa damu mwilini.

3. Huondoa Magonjwa ya Asubuhi
Licha ya kuwa tiba ya magonjwa kama Kikohozi na Mafua, Tangawizi pia husaidia kupunguza magonjwa ya asubuhi kama uchovu, na mning’inio. Kwa akina mama wajawazito, Tangawizi huwapunguzia homa za asubuhi pindi wanapoamka, pia hutumika kama kichocheo cha utulivu.

4. Mfumo wa Chakula
Husaidia mwili kunyonya virutubisho kwenye chakula. Hii husaidiana sana pale unapoamua kupunguza uzito wa mwili na kupata virutubisho vilivyo muhimu tu.

5. Kurekebisha Sukari ya Mwili
Tangawizi husaidia katika kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu. Wagonjwa wa Kisukari wanashauriwa kutumia Tangawizi badala ya chai.

6. Nguvu za Kiume.
Tangawizi pia inatawaja katika kuhimarisha nguvu za kiume ambapo unaweza kuitafua au kuichemsha au kutumia katika chai kutwa mara tatu.

7. Uzalishaji wa Mate Tangawizi
Unywaji wa Tangawizi husaidia uzalishaji wa mate mdomoni. Kuongezeka kwa mate mdomoni husaidia kutengeneza vichocheo Muhimu vinavyosaidia wakati wa kula, na hupunguza pia uwezekano wa magonjwa ya meno.

8. Kuyeyusha Mafuta
Tangawizi husaidia kupunguza Kuganda kwa mafuta mwilini ambayo yana madhara makubwa mwilini. Hasa magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu.

9. Kuondoa Sumu Mwilini
Tangawizi husaidia kupunguza kichefuchefu na kutapika. Pia huwasadia sana wale watu waliotumia sana madawa na kuwa na  sumu nyingi mwilini.

10. Tangawizi Pia humsaidia mtu mwenye vidonda vya tumbo kwa kupunguza maumivu na hata kuponya vidonda hivyo kama vitakuwa kwenye hatua ya awali sana!
  
11. Hamu Ya Kula (appetizer)
Huongeza hamu ya kula chakula. Kwa wale wenye mfumo mbaya wa umeng’enyaji wa chakula wanashauriwa kutumia tangawizi ili kupata mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment