KILIMO BORA CHA NYANYA MAGONJWA NA WADUDUU
tangulizi
Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili
hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya
kuridhisha ikilinganishwa na mazao mengine.Pamoja na umuhimu wa zao hili,
wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili
mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia
udhibiti wa magonjwana wadudu wa zao hili.Kipeperushi hiki kinatoa maelezo ya
udhibiti wa magonjwa na wadudu muhimu ya zao la Nyanya.
MAGONJWA YA NYANYA
Bakajani chelewa (Late blight)Ugonjwa huu huenenzwa na
vimelea vya fangasi. Husababishwa na hali ya hewa hasa ya unyevunyevu, na
huenezwa na upepo. Majani, shina, matunda hushambuliwa. Majani huwa na ukungu
mweupe na kijivu, na baadaye hukauka. Matunda huwa na mabaka ya kikahawia na
baadaye kuoza. Mashina pia huwa na mabaka ya kikahawia.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa ya kuzuia ukungu hasa wakati
wa masika, Dawa zinazopendekezwa ni Ridomil, Dithane 45, Bravo, Funguran,
milraz
.• Fanya mzunguko wa mazao. Usipande nyanya sehemu moja kila msimu au
palipolimwa mazao jamii ya nyanya km viazi mviringo, bilinganya, aina zote za
pilipili na nyanya chungu.
• Tumia mbegu safi
• Panda aina za nyanya
zinazovumilia ugomjwa
Bakajani tangulia (Early blight)Huenezwa na vimelea vya
fangasi. Husababishwa na kuenezwa na hali yahewa pamoja na mbegu zenye ugonjwa.
Mabaka ya kahawia yenye mistari ya mviringo huonekana kwenyemajani na shina.
Baka jeusi hutokea sehemu ya tunda inayoshikana na kikonyo.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa ya Kocide, Funguran
• Teketeza
mabaka ya mazao baada yakuvuna
• Tumia mbegu safi na bora
Mnyauko fusari (Fusarium wilt)Huenezwa na mbegu zenye
ugonjwa. Husambazwa na vimelea vya fungasi vinavyoishi kwenye udongo.Ugonjwa
hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi. Vimelea hushambulia sehemu au mirija ya
mmea ya kupitishia maji na chakula. Mmea hukosa maji na chakula na hatimaye
hunyauka. Shina la mmea likipasuliwa ndani huonekana rangi ya kikahawia.
Udhibiti
• Tumia mbegu safi na bora
• Tumia mzunguko wa
mazao. Nyanya zisizungushwe na mazao jamii yake
• Teketeza masalia ya mimea
•
Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Mnyauko bacteria (Bacterial wilt)Ugonjwa husababishwa na
vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye udongo. Huenezwa na kusambazwa na mbegu
na udongo wenye vimelea. Mirija ya mimea ya kupitishia maji na chakula
hushambulia na mimea hunyauka ghafla. Mmea hukauka na kufa.
Udhibiti
• Panda mbegu safi
• Panda nyanya sehemu
ambayo haijawahi kupandwa viazi mviringo, bilinganya au nyanya chungu
• Tumia
mzunguko wa mazao
• Hakikisha mfereji wa maji ya kumwagilia hayapiti kwenye
shamba lenye historia ya ugonjwa huu.
• Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia
mbegu Mnyauko vetisili (Verticillum wilt)Hakuna dawa inayozuia au
kutibu ugonjwa huu kwa sasa. Ugonjwa husababishwa na ukungu (fangasi) kwenye
udongo. Ukungu huu huishi kwenye udongo kwa muda mrefu bila kudhurika. Ugonjwa
huongezeka ikiwa mizimizi ya nyanya imeshambuliwa na minyo fundo; au kukiwepo
na hali ya ubaridi au ukame. Ugonjwa husababisha hasara kubwa. Ugonjwa
hushambulia sehemu ya ndani ya shina na kusababisha sehemu hiyo kuwa na rangi
ya kijivu. Majani hugeuka njano na mime kunyauka na kufa.
Udhibiti
• Tumia mzunguko wa mazao usiopungua miaka
mine
• Ondoa mabaki ya nyanya shambani• Tumia mbegu bora na safi
Bakadoa (Bacterial spot)Ugonjwa huu huenezwa na vimelea vya
bacteria vinavyoishi kwenye mbegu, pia kwenye hewa. Huenezwa kwa kasi sana
wakati wa masika. Madoa ya rangi kahawia huonekana kwenye majani na matunda.
Udhibiti
• Panda mbegu bora na safi• Tumia mzunguko wa
mazao
• Teketeza masalia ya mazao
• Nyunyizia dawa ya funguran, Kocide101, Cobox,
Bravo
Makovu bakteria (Bacterial canker) Ugonjwa huenezwa na
vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu nahewani. Hutokea zaidi wakati wa
masika. Majani hukauka nchani na makovu yaliyodidimia hutokea kwenye shina.
Matunda huwa na makovu yenye rangi ya kahawia sehemu ya katikati.
Udhibiti
• Tumia mbegu bora na safi
• Teketeza masalia
ya mazao• Tumia mzunguko wa mazaoRasta (Yellow leaf curl)Ugonjwa huu
husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Hutokea zaidi wakati wa
kiangazi. Mimea hudumaa na majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya manjano na
pengine rangi ya zambarau. Nyanya hupasuka.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa za sumu za kuua wadudu
(Selecron, Dursburn, Actelic)
• Ng’oa mimea yenye ugonjwa
• Tumia mzunguko wa
mazao
• Weka shamba katika hali ya usafi
Batobato (Tomato mosaic virus)Ugonjwa husababishwa na virusi
na hueezwa na mbegu na kugusana. Majani huwa na mchanganyiko wa rangi hasa
kijani kibichi na kijani kilichofifia (majano). Majani hujikunja na manjani
machanga huwa na maumbile yasiyo kawaida. Ukifikisha jani huwa
linavinjikavunjika.
Udhibiti
• Tumia mbegu bora na safi
• Ng’oa mimea
iliyoshambuliwa
• Teketeza masalia ya mazao
• Weka shamba katika hali ya usafi
WADUDU WAHARIBIFU
Viwavi Matunda (Fruit worm) Viwavi hawa hutokana na wadudu
nondo. Viwavi hutoboa matunda na kuacha matundu na hatimaye matunda
huoza.Hupunguza ubora wa matunda.
Udhibiti:Nyunyizia dawa ya kuua wadudu. Dawa hizo ni
pamoja na Actelic 50EC, Selectron, Dursbaan, Maji ya majani yamwarobaini au
utupa pia huua wadudu.
Utitiri wekundu (Red
Spider mites) Hawa ni wadudu wekundu, wadogo sana wanaoweka utando chiniya
majani, hasa wakati wa kiangazi. Wadudu hawa hufyonza utomvu kwenye majani na
kusababisha majanikukauka.
Udhibiti• Nyunyizia dawa za sumu. Dawa hizo ni pamoja
na Actellic, Selecron, Dursbarn na Thionex• Mwagilia maji mara kwa mara• Weka
shamba katika hali ya usafiInzi weupe (White flies)Hawa ni Inzi weupe wadogo
sana. Hujitokeza sana wakati wa kiangazi. Hueneza ugonjwa wa virusi ujulikanao
kama Rasta.
Udhibiti:Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama
Selecron, Actellic, Dursban na thionex. Pia maji ya majaniya mwarobaini na
utupa.Vidukari au Wadudu mafuta (Aphids)Ni wadudu wenye rangi nyeusi au kuijani
au kahawia. Hukaa chini ya majani na kufyonza utomvu kwenye majani machanga.
Hudumaza mmea na kushindwa kuzaa matunda
Udhibiti:Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama
Rogor, Actellic, Selecron, Dursban maji ya majani ya mwarobaini na utupa, maji
ya pilipili.
Minyoo (Nematodes)Ni minyoo midogomidogo ambayo hushambulia
mizizi na kuweka vifundo. Mizizi hushindwa kuchukua maji na chakula kwenye
udongo. Mimea hudumaa na kushindwa kuzaa
Udhibiti
• Tumia mzunguko wa mazao
• Choma udongo wa
kitalu kabla ya kusia mbegu kwa kutumia karatasi la plastiki jeusi na nishati
ya jua
• Choma masalia ya mazao
Sota (Cutworms)Hushambulia miche ya nyanya hasa baada ya
kupandikizwa shambani. Wakati wa mchana hujificha kwenye udongo na usiku
hujitokeza na kukata miche kwenye shina usawa wa udongo.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa za kuua wadudu kwenye shina
usawa wa udongo
• Hakikisha miche inapata maji ya kutosha.
0 comments:
Post a Comment