UFUGAJI BORA WA KUKU WA NYAMA NA MAYAI:
Wiki ya Kwanza: Siku ya 1 – 6, Wape: glucose broiler boost au aminovit au super vitvigo start kwenye chakula (kilo 1 kwa mfuko 1 wa kg 50) kuanzia wiki ya kwanza hadi ya 4.
Siku ya 7: Chanjo ya newcastle - masaa 2 tu, weka maji na vitamin mara baada ya kutoa maji ya chanjo.
Wiki ya pili: Chanjo ya gumboro - masaa 2 tu, halafu endelea na maji ya vitamin.
Wiki ya tatu: Doxicol au ctc20% na amprolium, vitamin na molasses kwa siku 5 - 7.
Wiki ya nne: Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dose kubwa ya vitamin.
Wiki ya sita: Wape kuku wa nyama maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni.
Wiki ya nane: Wape kuku wa mayai chanjo ya ndui, dawa za minyoo (piperazine au lekiworm) vitamin au supervit layers walishe growers mash au farmers concentrate hadi miezi 3 na 1/2 tumia layers mash wakifika miezi 4 kamili au wape majani.
Wiki ya kumi na mbili: Wape chanjo ya newcastle (rudia kila baada ya miezi 3) masaa 2 kisha wape maji ya vitamin.
Wiki ya kumi na sita: Kata midomo kisha wape neoxyvital kwa siku 3-5 andaa viota.
Wiki ya 54: Wape virutubisho vyenye kuongeza wingi wa mayai mfano glp (kilo 1 kwa kila kilo 50 za chakula, wiki ya kwanza na nusu kwa wiki zinazofuata na vitamin.
Wiki ya 72: Tumia v rid kusafisha mabanda ili kuua vijidudu pia weka maji ya dawa hii kwenye dish ya kusafishia miguu (footbath) ili kuhakikisha udhibiti wa vijidudu (biosecurity) na kwamba vifaranga wanaowekwa hawaathiriwi na vijidudu hivyo.
Wiki ya 96: Ondoa kuku wote waliozeeka
0 comments:
Post a Comment