Ulishaji wa mifugo
kwa njia ya “HYDROPONICS SYSTEM”
Huu ni mfumo wa kilimo ambao mmea unapandwa bila kutumia
udongo, kilimo hiki kinatumika sehemu ambayo haifai kulima kilimo cha
kukwatuliwa na jembe, ili kuzalisha mazao mengi.
Kwa kutumia kilimo hiki tunaweza kuzalisha chakula bora na
bei nafuu kwa mifugo mbalimbali kama vile kuku, bata, ng’ombe, mbuzi, kondoo na
mifugo migineyo.
Mbegu bora za ngano, mtama au mahindi zinaoteshwa sehemu
ambayo imeandaliwa kuoteshwa kwa ajili ya kulishia mifugo.
Kutengeneza chakula cha mifugo kwa mfumo huu kuna faida kwa
mfugaji kama vile mifugo inaogeza uzito na uzalishaji wa mayai, kwa ng’ombe
hutoa maziwa mengi, pia hata nyama yake inakuwa nzuri na bora.
Pia vifaa vinavyotumika kutengeneza mfumo mzima wa
“Hydroponics” ni gharama ya chini kulinganisha na mifumo mingine ambayo mfugaji
anapashwa kutumia fedha na muda mwingi kununua chakula na kupeleka mifugo
porini kwenye machungio.
Mfumo wa hydroponics ni rafiki wa mazingira pia kuokoa fedha
nyingi za mkulima na mfugaji.
0 comments:
Post a Comment