MAMBO MUHIMU KATIKA KILIMO CHA NANASI

Hali ya hewa


Nanasi zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita 1300 hadi 1750 hufaa zaidi kwa uzalishaji kwaajili ya kusindika na mwinuko chini ya hapo hufaa zaidi kwaajili ya ulaji wa moja kwa moja Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C
Udongo
 Hustawi vizuri katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga usiotuamisha maji
Maandalizi ya shamba
  •   Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45
  •   Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa senti mita 120 (futi 3) hadi sentimita 150 (mita 1.5) kutoka kati ya tuta na tuta 
 Upandaji
  •   Zipo aina mbali mbali za ‘mbegu’ (machipukizi/maotea) lakini yale yanayochipua kutoka ardhini hufaa zaidi na hukomaa mapema. Chagua machipukizi mazuri yenye umri mdogo na yenye kulingana kwa ukubwa
  •   Punguza majani na mizizi yake na kisha yaache yakinyauka juani wa siku tatu hadi saba, hii huzuia vimelea vya magonjwa kuambukiza wakati wa kupanda
  •   Kisha pima mashimo ya kupandia katika umbali wa sentimita 50 hadi 60 kutoka shina hadi shina katika     mfumo wa zig-zag pande zote mbili za tuta na kuacha upana wa sentimita 60 (futi 2) kati ya msitari na msitari katika tuta
  •    Weka Mbolea kianzio katika kila shimo na kupanda 
  •  Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda 
Palizi
  • Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu 
  •  Magugu hudhibitiwa kwa palizi  ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. 
  •  Matumizi ya viuagugu hurahisisha zaidi palizi ya nanasi ukizingatia kuwa nanasi huwa na miiba katika ncha za majani yake ambazo huchubua ngozi endapo palizi za jembe zitatumika. Njia nyingine ni matumizi ya plastiki maalum kuzuia magugu yaani plastic mulch 
Mbolea
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda, UREA mwezi mmoja baadaye na kisha tumia NPK 20:10:10 kila baada ya miezi 3 kwa maelekezo na ushauri wa wataalam 
Matumizi ya viuatilifu 
Nanasi ni zao lisilosumbuliwa na wadudu ama magonjwa mara nyingi. Hivyo endapo patatokea mashambulizi ya wadudu na magonjwa ushauri zaidi wa kitaalam utafutwe kukabiliana na tatizo husika
 Mavuno
 Mavuno ya nanasi huanza baada ya kiasi cha miezi 15 hadi 24 tangu kupanda kutegemea na aina ya maotea ya mbegu yaliyotumika  
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment