
Morning Rise Up
✍🏽"Ongeza thamani yako "

Unapoenda sokoni au
dukani unakutana na vitu vingi ambavyo huuzwa kwa bei tofauti .Utashangaa nguo
hii inauzwa kwa bei kubwa kuliko nguo ile .Hii ni kutokana na material
(thamani ) ya vitu vilivyotengeneza nguo hiyo.

Hata hivyo thamani
ya kitu inaweza kuongezwa na mtu mwenyewe , kwa mfano ukikuta mtu anauza nyanya
na akawa ameziweka kwenye mifuko maalumu (Packaging) bei yake itatofautiana na
mtu aanyeuza nyanya na hajaweka kwenye mifuko maalumu.

Mazingira pia
huongeza au kupunguza thamani ya kitu .Kwa mfano bei ya nguo inayouzwa kariakoo
ni tofauti na ile ya Mlimani City .Hii ni kwa sababu mazingira ya mlimani city
yana thamani kubwa kuliko mazingira ya kariakoo .

🏼Ni bahati
mbaya kwamba watu wanapenda vitu vya thamani wakati wao hawana thamani na
hawapendi kujiongeza thamani .Mtu anavaa nguo ya thamani kubwa wakati thamani
yake ni ndogo kuliko nguo aliyovaa.

Heshima yako
haitaletwa na Boss wako wala miujiza ya kuombewa lakini ni kwa kutafuta jinsi
ya kuongeza thamani mahali unapoishi .Unadhauriwa kwa sababu huna thamani(you
don't add any value).Umebaki unalipwa hicho unacholipwa kwa sababu
thamani yako kila siku haiongezeki.

🏾Wewe ni
kama bidhaa iliyoko sokoni , bidhaa ili ziuzike vizuri zinaongezwa thamani
.Bidahaa inafutwa vumbi ,bidhaa inapangwa vizuri ili tu iweze kuuzika vizuri
vinginevyo bidhaa haitauzika.

�Ili maisha yako
yawe ya thamani lazima ujue namna ya kuongeza thamani katika maisha yako .Uko
hivo ulivyo,unalipwa hivyo kwa sababu thamani yako ni ndogo sana na huna mpango
wa kuiongoza .

�Thamani ya maisha
yako ianaongezwa kwa kusoma vitabu vyenye kuongeza maarifa(siyo udaku).Tunza
ulimi wako usiwe mtu wa kuropoka tu (Jua wakati wa kuongea ). Chagua marafiki
wa kuongeza thamani siyo wambeya wanaoongea maisha ya watu .Acha mizaha ili
uongeze thamani yako.
Jelous ()
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment